UKWELI TIBA.

Monday, January 30, 2006

Rudi! Rudi Mwanangu Rudi!

RUDI!RUDI MWANANGU RUDI!

Rudi nyumbani mwanangu rudi
Rudi nyumbani pombe yakutosha rudi
Rudi Ukimwi hakuna Rudi
Rudi ! Rudi Mwanangu Rudi

Usifikirie Vinginevyo
Mimi Mzaziyo naomba rudi
Nakupenda Mwanangu Rudi
Rudi! Rudi Mwanangu Rudi

Swali Mwanangu jibu
Hivi ulipata hivyo na ukakosa vyote
Umepata kitu gani?
Rudi!Rudi Mwanangu Rudi

Najua wajua elimu unayo
najua wasema ulimwengu ni wako
Lakini wewe ni Dunia?
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Mwanangu watofautisha visa
Dhambi wasema makosa
Kisa eti makosa hukumu ni papo
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Dhambi eti ni Hukumu mpaka Mungu
Acha basi uishi pasi kujificha ficha
Rafiki zako mpaka uwe nazo?
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Nakupenda mwanangu nakupenda sana
Ugenini wapata taabu sana
Waishi kama kima;wafanya kazi kama punda aliyekodiwa
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Kisa kwa kuvaa nguo za kisasa na kuwa na...
Na usalama wako je?si ardhini au angani
Popote waweza kupata ajali
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Najua wanikumbuka Mwanagu
Najua wanipenda Mwanangu
Lakini kwa nini unakaa kimya
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Kwa nini Mwanangu......?
Mwanangu......
Itikia basi Mwanangu.....
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Mwanangu.......Africa


2 comments:

FOSEWERD Initiatives said...

nimelipenda shairi....linaelezea hisia za mzazi anayetaka kuunganika tena na mwanae.

nyembo said...

mh!
mwakeye e mugabho!
nimefurahi sana kuona unatoka huko kasulu na kutufikia sote katika ulimwengu huu, nafurahi pia kuweka yangu machache hapa baada ya kugundua kuwa unao uwezo mzuri wa kutunga. nakuahidi kuandika beti kadhaa kuonesha furaha yangu, na ninakukaribisha