UKWELI TIBA.

Wednesday, February 01, 2006

Tutapona?

Mungu najua yote! Nadhani kwangu ndio jibu sahihi kwa swali linaloulizwa na watu kwa sasa kila siku kutokana na balaa la njaa linalonyemea taifa late ua tusema ambalo linaliandama taifa letu.

Hapa Kasulu mvua zinanyesha karibu kila siku lakini sikiwa zimechelewa sana;na zinanyesha kwa namna ya ajabu sana....yaajabu sana kwani ndani ya wilaya hii ya Kasulu kuna sehemu mvua haijanyesha kwa wiki sasa na mahindi ambayo yalichelewa kupandwa yaanza kukauka,Kweli Tutapona?

Maajabu mengi!Wilaya ya kasulu inarutuba ya kutosha sana lakini ardhi ilimwayo ni nadhani hata robo ya hiyo yenye rutuba ndio ilimwayo...Kwani jembe bado ni la mkono kwenye ardhi ngumu sana na Wilaya nzima ina trekta moja tu (nimeambiwa sijawahi liona likilima)
Kasulu inaongoza kwa mkoa wa Kigoma kulima mazao ya chakula (ajabu) Haina hata hatua mbili ya barabara ya lami au ya kutumika majira yote.

Ajabulingine kelele:Kwangu naweza sema ndio Wilaya yenye kelele kuliko zote kwa hapa Bongoland(Tanzania).Kwani kila upitapo vichochoro vya Kasulu kuna Jenereta au kajenereta kama wenyeji wasemavyo kila kitu weka mwanzo neno (ka) linaunguruma na kuachia moshi mchafu sana.
Wenyeji wana sema ukija umeme tutakuwa nchini na sisi.....Nina hakika hawana taarifa za gharama za umeme wa TANESCO ziendazo kasi kama....taja wewe!

Sahamani rafiki yangu Philipo! yeye uamini ongezeko la watuhasa kwenye famila yao ni kutokana na kukosekana kwa umeme na barabara bora.Ni kweli?Malizia---------------------

Tutapona kweli? hakuna miundo mbinu Tata.....kweli akili zetu na hata kwenye mazingira yetu.Kwani kila kijana anafikiria kutoka na kila mwenye Usiasa anafikiria kuwa fulani kwenye sehemu fulani hata kwa Uchawi(nimekosa neno ...sahihi)Ila sijui wewe wataka kutokaje.....
Kuana rafiki yangu Kule KAHAMA uamini kwamba nchii hii kila mtu akipewa anachotaka mambo yatakuwa safi.....Wape bangi watakao....Kwani unadhani wanaongoza hawajui wapi inatoka......Wape Wazinzi.....Wape Rushwa.....Nawe?

1 comment:

FOSEWERD Initiatives said...

mwalimu. kuna baadhi ya mambo sasa ilibidi yafanyiwe marekebisho ili tuende mbele. umezungumzia kasulu yenye neema tele...lakini kulikoni? leo hii wizara ya miundo mbinu kuanza tu, wanajadili safari ya kwenda kigamboni kuwa je ipitie daraja au kuongeza pantoni?

swali langu mimi ni kwamba. kwa nini tunapofikiria chochote basi ubongo wetu wooote uruke hadi dar?

hata hivyo, mimi nadhani serekali za majimbo zinazoongozwa na mawaziri wakuu / magavana zingeweza kuwa jibu. CHADEMA walilihubiri hili kwenye kampeni ikachukuliwa kuwa ni ukabila. hii ingefanya kwa mathalani, nchi ikakatwa kama vipande sita hivi na cha saba visiwani, halafu kila jimbo linapambana kuzalisha na kuendeleza watu wake pia miundo mbinu...panapozidiwa serekali kuu inaingilia....sijui unalionaje hilo...madini yetu ya kigoma yakajenge majumba dar?