UKWELI TIBA.

Tuesday, February 07, 2006

SISI NI WAVIVU?

Kweli sisi ni wavivu? Yaani sisi Watanzania.Inawezekana kweli kwani mpaka sasa bajeti ya nchi yetu inatoka ng'ambo.Kila kitu tunacho...ardhini,majini na hata watu wapo(tupo).

Kuna rafiki yangu anajibu swali hili kwa kusema walioko madarakani tangia unaoitwa Uhuru ni mwezi na walafi na wanalaghai na waongo.Wegina yeye anasema wote si viongozi wema!kama wapo wachache sana.Na damu yetu iwe juu yao.

Ni wavivu! kutokana na hoja hizo mbili kwani hakuna hata miongoni mwetu sisi yaani wenye nchi anaonesha kukerwa kweli kweli na jambo hilo la kuishi maisha duni na yasiyo na matarajio kwa familia yako(zetu).

Hakuna hata maandamano hata milio ya makelele...hakuna hata risasi za amani yaani maneno ya kweli kama risasi pindi yatokapo mpata yule anayeambiwa hayo maneno ajue kweli kweli hasipo sikie yatamjeruhi au kuua kabisa(INDIA inawezekana kwanini kwetu tusiweze?)

Tuamua sasa wakati ukifika hakuna hatayekuwa salama hata kama ukifa yawezekana maiti yako isizikwe ndan ya kaburi.

Eti Sisi tunaongea sana?



SISI kweli ni wavivu

6 comments:

Reggy's said...

Sisi si wavivu. Tuna njaa. Mwenye njaa hata kwenda kuomba chakula hawezi, kwenda kulima hawezi, kwenda shule hawezi, hata akifa kama amezungukwa na wenye njaa wenzake kuzikwa kwake ni vigumu. Kama hali iko hivyo, tutawezaje kukataa hali tuliyonayo hata kama tuna nia. Tutaendaje kuandamana wakati tumboni hamna kitu na vichwani mwetu hana kitu. Tutawezaje, wakati watawala wetu wameunda majeshi ya kuwasaidia na kudhibiti wananchi wasiandamane dhidi yao? Ukiandamana ukaumizwa utapataje fedha ya matibabu wakati una njaa? Ukiwekwa lupango, utatokaje bila wakati ni mwenye njaa? Ukifunguliwa kesi utashindaje kesi wakati una njaa? TAFAKARI

FOSEWERD Initiatives said...

KUNA KITU KIMOJA....NADHANI NDIO KAZI KUBWA YA blogu hizi....mimi huamini katika kichwa kichwa ikiamka kila kitu inatia adabu....

kupambana na hili inabidi kuamka wale wachache waliopata mwanga wawaelekeze wenzao...tujue jinsi ya kupita na nini cha kufanya...mwenzio akaweka duka la unga na wewe unaweka lako la unga pembeni si kuanza kurogana? kwa nini usiweke la kitenge?? je uvivu kufikiri au kutokujua??

waliopata nafasi ya kuona mbele na wakapewa nafasi wawamulikie na wenzao...lakini swali hapo je nani aliwakabidhi tochi?? waliipata kihalali?? je watajitahidi kuona kuwa kila mara betri ziko gado?? je wanajua kwanini tumewapa kurunzi...

wanasema nchi jhujengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye choyo...tukisema hayaishi...kila mara atapotokea mtu wa watu mtu mwema kale ka usemi kuwa wema hawana maisha....yuko wapi moringe? yuko wapi mrema?? na wale waliowamaliza ndio hao tunawaona na tunawapigia makofi na wengi wao tumewarudisha madarakani...kupiti hii kasi mpya na ari mpya...wengine wamestaafu tena kwa heshima kubwa tu.....

tunatakiwa kujirekebishe, tupendane na tuelekezane...CHA MSINGI TUAMKE NA TUFANANE NA TAIFA LA WATU WANAOTUMIA KICHWA, WANAOJUA HAKI ZAO ZA MSINGI NA HUO NDIO MWANZO!!

Mija Shija Sayi said...

Bado nalitafakari suala hili, linahitaji utafiti wa kina hasa ili kujua tatizo ni nini.

Vempin Media Tanzania said...

Damija

Unalosema ni la kweli kabisa kwasababu wanafalsafa wanasema huna haki ya kuzungumza kama hujafanya utafiti basi nami pia nalitafakari suala hili ni zito. Hivi kweli sisi ni wavivu? Au kuna kitu kingine kinachotufanya tuwe hivi.

Sultan Tamba said...

Mimi nafikiri tunaongozwa na wavivu, lakini sisi wenyewe tumechangamka. Viongozi ndio wa kuwafanya watu wasiwe wavitu lakini kama wao wanatunga sheria za kufanya watu wawe wavitu wanategemea nini. Uhajaribu kufuatilia leseni ya biashara leo? Jaribuni ndio mtaelewa kwamba zinatungwa sheria za kufanya watu wawe wavivu.

Reggy's said...

Kweli sisi ni wavivu. Tangu uweke makala hii muda umepita, umeamua kulala kabisa bila taarifa. Si dalili za uvivu hizo?. Au una sababu naomba utuarifu wenzio tunakutembelea tunakuta olaaaa.