UKWELI TIBA.

Wednesday, December 20, 2006

MWISHO WA RELI-PICHANI

KIGOMA

NI SEHEMU TU YA KIGOMA PICHANI

Ni mwisho wa reli.Ni msemo ambao niliusikia takribani miaka zaidi ya Ishirini(20) na ushee tangia niishi hapa Tanzania;ndio hapa Tanzania?! na sio Tanganyika iliyotimizi miaka 45 ya Uhuru wake toka chini ya makucha?Tunamiriki maliasili zote sisi wewe?
Kuanzia Mara mpaka Mtwara ukipitia njia zote za lami majira yote ya mwaka.

Ndio Tanzania Bara?Watoto wake wanajua Uvinza kuna chumvi,Mikumi,Serengerti na Bonde la Moyowosi kuna wanyama pori na Gombe kuna Sokwe mtu.......Lakini atafikaje? kwani kutoka Tanzania mpaka Kigoma ni siku si chini ya tatu?

Mazingira yake yanachomwa sana kwa moto na acha hukataji wa mti.Niko huku sasa ni mwaka wa tatu nimeshaambiwa si na mtu mmoja ...........una ona ule mlima pale.....ule kule kuliko na msitu na wanyama pori kibao(wengi sana).

Wakimbizi walipoingia..............mafuta ya taa yaliporipuka bei...na sio kupanda;kwani zaidi ya asilimia 97 ya wenyeji wanatumia kuni?

Monday, October 09, 2006

UTATA?

UTATA?
Safari ya kutoka Kasulu mjini kuelekea Dar es salaam yaanza kupitia Kigoma Mjini kwa usafiri wa Basi,Treni,Basi na Teksi.

Kasulu kwapanda ndani ya basi na kusubiri Wasafiri wengine kwa muda wa masaa wawili kamili kisha gari laanza safari.Polisi ambaye kwa jina maarufu anaitwa Trafiki anatukamata mita 20 tu kutoka kituo cha mabasi hayo na kudai waziwazi chake(RUSHWA).

Gari kwa kweli alisitahili hata kidogo kuwemo barabarani......kuanzia bodi yake na mwishoni mwa safari na gundua hata dreva wake naye hastahili kuwemo ndani ya chombo hicho........NAAMBIWA MUDA WA GENERETA KUPUMZIKA UMEFIKA Baadaye.......

Monday, October 02, 2006

UWEZO NINAO?


Uwezo ninao?Ni swali ambalo kila siku kwangu ni ngumu sana kulijibu,kiasi ambacho naomba msaada kwenu ndugu zangu popote mlipo.Na bila shaka waza jiuliza uwezo gani hasa nataka pata msaada wa ndugu nisaidi.Si pesa au mali naomba nisaidieni.
Naipenda sana Tanzania......hilo ni la kwanza,Pili;nawapenda sana viongozi wetu wa Mtanzania,Tatu;Uwezo wangu wa kujua wapi Tanzania Tunakwenda(Mtarajio ya kisera)
Naipenda sana Tanzania;siwezi kuikimbia nchi yangu nzuri sana Tanzania.Tanzania ooh Tanzania ooh .....Una Maziwa ya maji yenye samaki ambao sisi hatuwezi kuvua kwa nguvu zetu ila uwezo wa kununua Mashingingi ya bei mbaya kwa kila kiongozi wa KAYA.....Sitawataja kwa majina yao( UWEZO NINAO?).


Ardhi yako Tanzania Ooh Tanzania ina madini mengi;ambayo hatuwezi kuyajimbua kama sio kuyajimba......Hata kufanya mikataba kuhusiana na madini hatuwezi.(UWEZO NINAO?)Najiuliza....Naomba jibu...Pengine sishibi ndio sababu ya kushindwa jibu swali hili.
PILI:Nawapenda sana viongozi wetu woooooooooooooooooote.Nawapenda kiasi ambacho sijui yupi ni mkweli....Kwangu ni kwamba wanaposema ni ukweli mtupu.....Mfano;HAKI SAWA,NI TAWAJAZA MAPESA,MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA NA SUALA LA UMEME(Na sio tatizo)SI MUDA LA MREFU:Nukuu ya Kiongozi wangu mpendwa wa nchi aha aha HAKUNA MTU ANAYEKULA SAMAKI WABOVU(MAPANKI).............

TATU:Matajio ya Kisera;KASI MPYA,ARI MPYA NA NGUVU MPYA.(UWEZO NINAO?)Nashindwa jua kama sera inaendana na vitu gani hasa?KASI MPYA.....kwenda wapi?ARI MPYA baaday ya hamasa gani hasa?NGUVU MPYA baada ya kula nini hasa?au baadaya kuwekewa mazingira gani ya msingi......Sio ujuzi wa sera.UWEZO NINAO? naomba msaada najua ndugu zangu ni wema kwani mtoto wangu akiuliza niweze kumjibu kwa ufasaha.

Tuesday, July 18, 2006

WOTE PIGA KOFI

Wote hatuna budi kupiga kofi;kwani dalili za maisha bora kwa kila Mtanzania sasa ni kweli.Umeme,barabara,ajira,na .......hewa safi kwa wote.

Maisha safi.....bila kofi Mtanzania...piga kofi kabla hawaja nunua RADAR,NDEGE NA KUJENGA JUMBA JINGINE LA BUNGE....SOMA THISDAY NEWPAPER LA MWEZI HUU
Piga Kofi Mtanzania....Usijali kama umeshiba ,au mtoto wako hatakwenda kweli shule.....ila kwa hili ondoa hofu shule kila kijiji na walimu bora wapo...

PIGA KOFI....hata kama hospitali ipo lakini hakuna Tabibu wa kutosha na dawa PIAGA KOFI hata kama kilimo cha mkono ni kama urithi wetu(WILAYA NZIMA YA KASULU INA TREKA MOJA LA PLAU)>>>>PIGA KOFI BILA KUSITA PIGAAAAAAAAAAAAAA KOFIIIIIIIII kabla hawajanunuliana magari mengine ya kifahari kwa ajili kupeleka watoto wao...hapana wetu shule......

PIGA KOFI MTANZANIA MWENYE NIA .......Hata kama vijana wetu wanakufa kiakili na kifikra kwa madawa ya kulevya yanayoletwa na Wahusika tusioweza kuwakamata ingawa wapo......

PIGA KOFI HATA KAMA UJUI LEO UMESHIBA KWELI AU LA>>>>>Kwa hili pia ondo shaka hakuna Mtanzania atayekufa kwa njaa ...ili tamkwa awali.

PIGA KOFI >>>>

Tuesday, July 11, 2006

Maisha?


MAISHA?
Maisha ni nini
?na je?thamani yake ni sawa kwa watu wote? hapana?......kweli?...Mimi kwa upande wangu ni ngumu sana kuamua.Wengine wana sema maisha ni kula na kunywa....?Wengine na wanawake....wengine wanajibu maisha ni mbinguni.hawa ni wale Waumini yaani waamini uwepo wa MUNGU WAO!

Maisha ni magumu sana.....maisha POA....na wengine watasema Maisha kwa sasa ni magumu sana.....kwa vigezo mbalimbali kila mtu nafasili yake kuhusu maisha .....lakini ni kweli iko hivyo?
Kaka yangu alfred... nukuu yake ....MAISHA SI MAGUMU KAMA TUNAVYOYAONA NA KUFIKIRIA....NI MAGUMU ZAIDI!!

Zaidi! Kuna watu wanakula maisha yao! Ndio yao! Wao wana kila kitu ...magari mazuri,vyakula vizuri,wanawake wazuri,wanalala pazuri na hata kufa wanakufa vizuri....nukuu ya MUKAMA MAKONGO.
Lakini hata kufikiri wanafikiri vizuri....bado ninatatizwa na MAISHA?
Nitaweza kuonekana kwa kitambo kwenye blogu sababu hasa ni maisha...kwa tafasili isiyo rasmi....!
MAISHA?

Tuesday, February 07, 2006

SISI NI WAVIVU?

Kweli sisi ni wavivu? Yaani sisi Watanzania.Inawezekana kweli kwani mpaka sasa bajeti ya nchi yetu inatoka ng'ambo.Kila kitu tunacho...ardhini,majini na hata watu wapo(tupo).

Kuna rafiki yangu anajibu swali hili kwa kusema walioko madarakani tangia unaoitwa Uhuru ni mwezi na walafi na wanalaghai na waongo.Wegina yeye anasema wote si viongozi wema!kama wapo wachache sana.Na damu yetu iwe juu yao.

Ni wavivu! kutokana na hoja hizo mbili kwani hakuna hata miongoni mwetu sisi yaani wenye nchi anaonesha kukerwa kweli kweli na jambo hilo la kuishi maisha duni na yasiyo na matarajio kwa familia yako(zetu).

Hakuna hata maandamano hata milio ya makelele...hakuna hata risasi za amani yaani maneno ya kweli kama risasi pindi yatokapo mpata yule anayeambiwa hayo maneno ajue kweli kweli hasipo sikie yatamjeruhi au kuua kabisa(INDIA inawezekana kwanini kwetu tusiweze?)

Tuamua sasa wakati ukifika hakuna hatayekuwa salama hata kama ukifa yawezekana maiti yako isizikwe ndan ya kaburi.

Eti Sisi tunaongea sana?



SISI kweli ni wavivu

Friday, February 03, 2006

MIMI SENEGAL

Mimi Senegal bwana....!Mimi DRC Congo na mimi ni......

Hayo ni baadhi ya maneno ya watazamaji(Watanzania).Ndio sisi ni watazamaji wa kudumu wa mashindano yeyote yale hapa duniani.

Sisi ni watazamaji na sisi sio Watanzania katika jambo la kushangilia na kushabikia mashindano hapa duniani.Usikatae kabisa hata wewe kama sio Manchester basi ni Liverpool kama Mimi....Mimi ni Liverpool!MIMI NI LIVERPOOL!

Kwenye utandawizi ndio Utandawazi (kama Tafsida) ukweli ni utandawazi kila mtu (hana) haki ya kupenda apendacho mradi kwake ni kizuri....Kwenye utandawazi hata Wabunge kujiongezea mishahara yao Ruksa kabisa....Unabisha nini?1

Hata Serikali kutoa ahadi ruksa hata ukibisha haisaidiee kitu.....Mimi Liverpool Fan( hapa mshangiliaji)......ETAENDELEA

Thursday, February 02, 2006

NINGE...

jana sio juzi!Ninge....Kamwe hakui kabisa.Maisha yako ukiyafananisha na ya fulani ;basi wewe sio wewe ila ni yeye.Hivyo basi hufai kuishi.Hapana Fulani mwenyewe hasiwe Yule ambaye jamii haimuhitaji kuwa naye!ISIWE FULANI KUWA WEWE!

Wednesday, February 01, 2006

Tutapona?

Mungu najua yote! Nadhani kwangu ndio jibu sahihi kwa swali linaloulizwa na watu kwa sasa kila siku kutokana na balaa la njaa linalonyemea taifa late ua tusema ambalo linaliandama taifa letu.

Hapa Kasulu mvua zinanyesha karibu kila siku lakini sikiwa zimechelewa sana;na zinanyesha kwa namna ya ajabu sana....yaajabu sana kwani ndani ya wilaya hii ya Kasulu kuna sehemu mvua haijanyesha kwa wiki sasa na mahindi ambayo yalichelewa kupandwa yaanza kukauka,Kweli Tutapona?

Maajabu mengi!Wilaya ya kasulu inarutuba ya kutosha sana lakini ardhi ilimwayo ni nadhani hata robo ya hiyo yenye rutuba ndio ilimwayo...Kwani jembe bado ni la mkono kwenye ardhi ngumu sana na Wilaya nzima ina trekta moja tu (nimeambiwa sijawahi liona likilima)
Kasulu inaongoza kwa mkoa wa Kigoma kulima mazao ya chakula (ajabu) Haina hata hatua mbili ya barabara ya lami au ya kutumika majira yote.

Ajabulingine kelele:Kwangu naweza sema ndio Wilaya yenye kelele kuliko zote kwa hapa Bongoland(Tanzania).Kwani kila upitapo vichochoro vya Kasulu kuna Jenereta au kajenereta kama wenyeji wasemavyo kila kitu weka mwanzo neno (ka) linaunguruma na kuachia moshi mchafu sana.
Wenyeji wana sema ukija umeme tutakuwa nchini na sisi.....Nina hakika hawana taarifa za gharama za umeme wa TANESCO ziendazo kasi kama....taja wewe!

Sahamani rafiki yangu Philipo! yeye uamini ongezeko la watuhasa kwenye famila yao ni kutokana na kukosekana kwa umeme na barabara bora.Ni kweli?Malizia---------------------

Tutapona kweli? hakuna miundo mbinu Tata.....kweli akili zetu na hata kwenye mazingira yetu.Kwani kila kijana anafikiria kutoka na kila mwenye Usiasa anafikiria kuwa fulani kwenye sehemu fulani hata kwa Uchawi(nimekosa neno ...sahihi)Ila sijui wewe wataka kutokaje.....
Kuana rafiki yangu Kule KAHAMA uamini kwamba nchii hii kila mtu akipewa anachotaka mambo yatakuwa safi.....Wape bangi watakao....Kwani unadhani wanaongoza hawajui wapi inatoka......Wape Wazinzi.....Wape Rushwa.....Nawe?

Monday, January 30, 2006

Rudi! Rudi Mwanangu Rudi!

RUDI!RUDI MWANANGU RUDI!

Rudi nyumbani mwanangu rudi
Rudi nyumbani pombe yakutosha rudi
Rudi Ukimwi hakuna Rudi
Rudi ! Rudi Mwanangu Rudi

Usifikirie Vinginevyo
Mimi Mzaziyo naomba rudi
Nakupenda Mwanangu Rudi
Rudi! Rudi Mwanangu Rudi

Swali Mwanangu jibu
Hivi ulipata hivyo na ukakosa vyote
Umepata kitu gani?
Rudi!Rudi Mwanangu Rudi

Najua wajua elimu unayo
najua wasema ulimwengu ni wako
Lakini wewe ni Dunia?
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Mwanangu watofautisha visa
Dhambi wasema makosa
Kisa eti makosa hukumu ni papo
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Dhambi eti ni Hukumu mpaka Mungu
Acha basi uishi pasi kujificha ficha
Rafiki zako mpaka uwe nazo?
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Nakupenda mwanangu nakupenda sana
Ugenini wapata taabu sana
Waishi kama kima;wafanya kazi kama punda aliyekodiwa
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Kisa kwa kuvaa nguo za kisasa na kuwa na...
Na usalama wako je?si ardhini au angani
Popote waweza kupata ajali
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Najua wanikumbuka Mwanagu
Najua wanipenda Mwanangu
Lakini kwa nini unakaa kimya
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Kwa nini Mwanangu......?
Mwanangu......
Itikia basi Mwanangu.....
Rudi! Rudi Mwanamgu Rudi

Mwanangu.......Africa


nilikwenda bize

SAMAHANINI
Kwani nini nasema hivyo?naomba msamaha kwa kutokuwa nanyi tangia wiki moja hivi iliyopita pasi mawasilano nanyi.Huwa tuna sameheana sisi wa Wana wa Adamu.Ahsante sana.
Nikwenda bizeyaani shughuli zangu za kila siku ilifikia mahali amabpo sukiweza kufanya zote kwa mudawangu wa kawaida;kiasi ambacho hata muda wa mimi kuweza kuandika ninacho fikiri kuwa mdogo sana.Niliweza kufikiri ila kitendo hicho kilikwenda sambamba na kitendo kufanyika....aha aha ndipo nikajua nini hasa maana ya kwenda au kuwa bize.

Kama kawaida niliweza kuhudhuria burudani kadhaa hasa mashindano ya kombe la mataifa ya Africa(Tanzania wakiwa kama Watazamaji wakuu wa mashindano hayo)...Ndio mbona washangaa? Ndio kama watazamaji wakuu wa mashindano hayo kwani Taifa Stars?iko Huko? Naomba jina ilibadilishwe.....sababu ninazo tena nyingi sana sio mimi tu hata wewe moja ni neno taifa Stars..Kwani Kufikiri na kutendo kwao tofauti kabisa.

Wako Bize! na nini?

Wednesday, January 18, 2006

Dar mpaka Kigoma

FIKIRI:
Unaweza kujaribu kufikiri jambo mpaka ikafikia mahali ukajiona wewe kweli una akil sana. AH AHA lakini cha kusitajabisha pinde watu wanapojua kuwa unachofikiri waanza ulizana kweli jamaa yuko timamu?

Dar Mpaka Kigoma ni safari yangu mimi nilioianza 2003 mwezi wa 8 na tarehe 5 stesheni ya Gari moshi(treni) ya Jijini Dar es salaam.Ni masimulizi yatayojili kila siku kwako Mungu akiendelea kuwa nami katika dunia hii.

Masimulizi yatakuja yakiwa na matukio ya kweli kuanzia siku ya kwanza kuondoka nyumbani Dar-mpka kufika Kigoma hasa wilyani Kasulu.Kwa watu ambao nitawataja kwa majina naomba msamaha kwa hilo hasa tukio tukio utapolitafasili vinginevyo.Naomba ujue hii dunia matukio yote si ya kweli nikiwa na maana kwamba kwani hayana mwisho.Pia kwa sentensi iliyotangulia maomba usilete ubishi.

Najua kila mtu ana akili timamu(kufuatana na sikolojia ya Maendeleo ya Mwana wa adamu) akilelewa vizuri kabisa kabla ya tendo na baada ya tendo(......).

SAFARI YAANZA

))001:NDANI YA TEKSI KUELEKEA STESHENI-dreva ANTHONY
NUKUU:Mtu huchoka zaidi anapokuwa hana kabisa cha kufanya.
ANTHONYna msikani vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu aaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhhhh mara Mwanga anawanga na gari bila ubishi lakata kona na kupaki pembeni ya barabara.....Mwanga anasogelea gari na swali moja baada la lingine....Mara kijana Leseni yako iko wapi?...Kijana Bima yako mbona chakavu sana....imekwisha muda nini?...najiuliza kwani haisomeki !nashindwa sema kwanibado dakika 45 tu kwa ya muda wa kulipoti stesheni fika.....HASIRA ZA MNYONGE! kelele zake....!! Afande basi kijana atakuona akinifikisha stesheni..hakuna taabu!

Afande(Mwanga)alikubali kwani tulikuwa mita chache kutoka stesheni

Tuesday, January 17, 2006

Jana?

Jana Bwana!Kila mara utasikia mtu anasema kuhusiana na jana yake;Yaani jana yake yeye aliweza fanya nini au alishindwa fanya nini hapa chini ya jua.

Kila mara watu wengi hupenda sana jana yao na wengi pia uchukia jana yao.Inafikia hata wakati wengi huondoa uhai wao kwa sababu ya jana.Huwa najaribu sana kufikiria kuhusu jana yangu......naogopa sana kuwa JIZI(Mwendawazimu)...naona jana yangu ilikuwa nzuri sana lakini nani?nani?aliweza haribu jana yangu? Bila shaka si mimi hata hivyo nashindwa sema nani kwa jana yangu ila kama sio mwanasiasa basi ni wewe kiongozi wa dini au jamii....Unakataa ni wewe !Ndio wewe eh ehe unakataa nini?Wewe ndio unashindwa kukemea jambo mbaya ninapotokee mbele yako,Wewe unashindwa fanya jambo zuri kila siku...ndio unayanfa baadhi ya watu wanaokupenda walie kwa mambo yako.....
jana?jana yako umewafanya au hata imeweza haribu kabisa matumaini yangu...hata yako ya kuwa fulani....Jana yako inakufanya hata shuhuli unayofanya usiipende sana...
Naipenda sana jana yangu..ndio kama wewe unavyoipenda jana yako....jana yako imekufanya Jamii ikupende Ongera sana jana yako ndio inayokupa chakula ccvha kila siku na jamii yako.....

Jana yako inakufuata popote pale uendapo hata kama utajificha jamii yako inapokutafuta jana yako .Mpaka ndani ya .....Kaburi yako kwa heshima kubwa huku ukiacha Jamii yako inayokupenda na kukuenzi ukuharibu kwakukatili mkubwa jana yao.
Jana ?....

Sunday, January 15, 2006

bhalezee

Kigoma Weather


--------------------------------------------------------------------------------
at: 9:00 pm EAT F° C°

Currently:
22°

Partly Cloudy High: 26°

Low: 20°





· Text Forecast
· Get Yahoo! Weather on your desktop


5 Day Forecast

Today Tomorrow Tue Wed Thu 6-10 Day



Scattered Thunderstorms


High: 26°
Low: 20°


Scattered Thunderstorms


High: 25°
Low: 20°


Showers


High: 23°
Low: 19°


Scattered Thunderstorms


High: 25°
Low: 18°


Scattered Thunderstorms


High: 26°
Low: 18°
Extended Forecast

Harusi ya jana

HARUSI YA JANA
Jana nilialikwa harusini.Ongera sana maharusi na wote tuliouzulia harusi .
Kulichanganya sana kinywaji:kulikuwa na Coca cola,fanta nyeupe kama ziitavyo,nyeusi,passion,Sprite,tangawizi na nyingine nyingi.
ambacho kilikuwa kigeni kwangu kwenye harusi hiyo ni dada mmoja ambaya ndani ya muda wa masaa matatu ya sherehe hiyo aliweza kunywa soda 13.
Nasema kitu kigeni kwani sikuwahi ona kabla jambo hilo na huku akiwa na shauku ya kuendelea kunywa lakini bahati nzuri baada ya kula chakula kasi yake ya kuendelea kunywa ilipungua sana.Mimi nikaondoka .
Habari zilizojiri baadaye zilisema mpaka mwisho wa sherehe aliweza kunywa soda 23.
Harusi ya jana

Friday, January 13, 2006

bhalezee

bhalezee
Niko Kasulu.Kasulu kuna mambo yaani ajabu kwangu kwani sikuweza ona kabla ya mwaka huu.
Tarehe 1 ya januari ya mwaka 2006 usiku nilipata mwaliko wa kwenda kwenye pati moja maridadi sana.Unashangaa nini ?kusema maridadi sana! hata kasulu kuna pati maridadi sana.
Jamaa mmoja alikuja na kudumu cha lita kama siyo tatu basi mbili na wengine kama watano kwakiwa na chupa tupa za plastiki nao wakaingia.
Kweli kulikuwa na vinywaji na chakula cha kutosha....nilichoona sikutegemea hasa kwa wahiji wa watendaji.
Kwanza nilimwona jamaa mmoja akimimina soda ndani ya ile cupa tupu ya plastiki .Nikashikwa na shauku ya kutaka jua je?na wale wengine nao ndio matumizi yao?
Nikainuka na kumtafuta yule mwenye lita pili au sio mbili.... ah ah ah yeye nikamwona kwa macho weupi akiweka lita zake ndani ya mfuko huku ikiwa imejaa kama sio mvinyo basi maji ya bia ....Nikashindwa vumilia nika mtafuta mwenyeji wangu kulikoni kuhusiana jambo hili...cha ajabu hakushangaa kabisa ila akanimbia mbona ni jambo la kawaida sana.
Nikasogeza keyboard na..
Waelezee(BHALEZEE)

bhalezee

Sema!unatakiwa husema nini hasa kinachokusibu!Usipo sema nani atajua wewe una tatizo au upedezewi na jambo unalofanyiwa ni mbaya kwako.Sema(waelezee-bhalezee) wajua ni jambo mbaya sana kwako......
Sema kwa vitendo yaani onesha waziwazi kwamba unachosema au unavyosema unamaanaisha hivyo kweli.
Sio ooH oH unajua mimi sitaki jambo hili huku haoneshi kabisa kwa vitendo kwamaba jambo hilo linakukera sana.
BHALEZEE