UKWELI TIBA.

Wednesday, January 18, 2006

Dar mpaka Kigoma

FIKIRI:
Unaweza kujaribu kufikiri jambo mpaka ikafikia mahali ukajiona wewe kweli una akil sana. AH AHA lakini cha kusitajabisha pinde watu wanapojua kuwa unachofikiri waanza ulizana kweli jamaa yuko timamu?

Dar Mpaka Kigoma ni safari yangu mimi nilioianza 2003 mwezi wa 8 na tarehe 5 stesheni ya Gari moshi(treni) ya Jijini Dar es salaam.Ni masimulizi yatayojili kila siku kwako Mungu akiendelea kuwa nami katika dunia hii.

Masimulizi yatakuja yakiwa na matukio ya kweli kuanzia siku ya kwanza kuondoka nyumbani Dar-mpka kufika Kigoma hasa wilyani Kasulu.Kwa watu ambao nitawataja kwa majina naomba msamaha kwa hilo hasa tukio tukio utapolitafasili vinginevyo.Naomba ujue hii dunia matukio yote si ya kweli nikiwa na maana kwamba kwani hayana mwisho.Pia kwa sentensi iliyotangulia maomba usilete ubishi.

Najua kila mtu ana akili timamu(kufuatana na sikolojia ya Maendeleo ya Mwana wa adamu) akilelewa vizuri kabisa kabla ya tendo na baada ya tendo(......).

SAFARI YAANZA

))001:NDANI YA TEKSI KUELEKEA STESHENI-dreva ANTHONY
NUKUU:Mtu huchoka zaidi anapokuwa hana kabisa cha kufanya.
ANTHONYna msikani vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu aaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhhhh mara Mwanga anawanga na gari bila ubishi lakata kona na kupaki pembeni ya barabara.....Mwanga anasogelea gari na swali moja baada la lingine....Mara kijana Leseni yako iko wapi?...Kijana Bima yako mbona chakavu sana....imekwisha muda nini?...najiuliza kwani haisomeki !nashindwa sema kwanibado dakika 45 tu kwa ya muda wa kulipoti stesheni fika.....HASIRA ZA MNYONGE! kelele zake....!! Afande basi kijana atakuona akinifikisha stesheni..hakuna taabu!

Afande(Mwanga)alikubali kwani tulikuwa mita chache kutoka stesheni

1 comment:

FOSEWERD Initiatives said...

kwa kweli jinsi ya uendeshaji wa jeshi la polisi mie unanitia kichefuchefu....sina mengi sana ya kusema lakini pia ni huo mfumo wa polisi kugeuka wakusanya kodi! nadhani kuna haja ya kufanyia marekebisho mifumo yetu ya bima...na kupambana kufanya quality check (road worth) ya gari kila mwaka