Mimi Senegal bwana....!Mimi DRC Congo na mimi ni......
Hayo ni baadhi ya maneno ya watazamaji(Watanzania).Ndio sisi ni watazamaji wa kudumu wa mashindano yeyote yale hapa duniani.
Sisi ni watazamaji na sisi sio Watanzania katika jambo la kushangilia na kushabikia mashindano hapa duniani.Usikatae kabisa hata wewe kama sio Manchester basi ni Liverpool kama Mimi....Mimi ni Liverpool!MIMI NI LIVERPOOL!
Kwenye utandawizi ndio Utandawazi (kama Tafsida) ukweli ni utandawazi kila mtu (hana) haki ya kupenda apendacho mradi kwake ni kizuri....Kwenye utandawazi hata Wabunge kujiongezea mishahara yao Ruksa kabisa....Unabisha nini?1
Hata Serikali kutoa ahadi ruksa hata ukibisha haisaidiee kitu.....Mimi Liverpool Fan( hapa mshangiliaji)......ETAENDELEA
UKWELI TIBA.
Friday, February 03, 2006
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
8 comments:
Njili,
Karibu sana. Tena mno. Tuletee sauti yako ambayo huko nyuma tusingeweza kuisikia kutokana na kutokuwa na teknolojia hii. Kumbuka kuwa tunachofanya sasa ni kujenga msingi na kuandaa mapinduzi ya nyanja ya habari na mawasiliano.
Hapa safi sana yaani sasa nasomeka nami Kigoma. Sijafika huko lakini nikitua nitakuja kukusalimia maana tayari sasa nina ndugu Njili wa kufikia na kujadiliana kuhusu maendeleo ya Mburogu. Karibu sana na kweli tumefurahi kukupata kartika kipindi hiki ambapo Blogu zimekuwa Haki ya kila mwananchi.
Karibu Njili
Nafurahi kupata kampani. Nimeandika mambo kadha kuhusu Kigoma na Kasulu. Nilitoka huko hivi karibuni na nilikuwa naandaa machache juu ya huduma za mtandao bila umeme wa TANESCO, nikitumia uzoefu wa Kasulu na Kibondo. Karibu sana. Nikiwa huko natumia huduma ya mtandao pale Kasulu TTC. Naamini siku moja tutaonana.
MWALAYE!MWILIWE!
Karibu sana.Hata ndugu zangu wa pale Nyakanazi,Kibondo mpaka Nyantakara mpaka sehemu za Rusahunga,Runzewe Nyakahura wanapata sana mawasiliano haya ya Bilogu.
Karibu!
Haya sasa makubwa. Moto wa ukuaji wa 'mburogu' (machapisho tando) ni wa kasi ya ajabu au kama ile ya moto kondeni kwenye nyasi kavu. Karibu ndugu yetu walau tupate habari za migebuka na mawese kwani vitu hivi sasa ni adimu, ingawaje tulipokuwa navyo tulividharau.
Karibu sana
Karibu sana Njili,
Mada ya ushabiki ni nzito sana.Kimsingi unaweza ukadhani ni suala dogo tu linaloishia kwenye ubishi wa kijiweni n.k.Madhara ni makubwa,uzalendo huanza kuyeyuka kupitia matundu madogo sana.Karibu sana.
Karibu sana
Mimi Arsenal bwana!! na hata kama hutaki lakini Juve tumewaonyesha cha moto hata kama tukiishia hapo hapo, kwani nini bwana?? Tumemtanguliza Madrid itakuwa sisi!! hahahahaaaaaaaa
Karibu sana Njili, nimeipenda sana staili yako uliyoingia nayo.... maandishi mafupi mafupi lakini yenye maana, utadhani kandanda la pasi fupifupi lakini zina madhara kwa wapinzani
Post a Comment