bhalezee

UKWELI TIBA.

Sunday, July 08, 2007

Bajeti yangu nitaitangaza kila nipatapo Fedha.

Habari za bajeti Wananchi wenzangu?

Ujue nimeacha kutmia neno Watanzania kutokan arafiki yangu mmoja kusema watanzania ni wale wote
wananeemeka na maliasili za nchii Tanzania.wananchi ni wale wote wanaishi kwenye nchi Tanzania pasipo kuneemeka nayo.(UCHOYO NA UNALAFIKI).

Watanzania wamesha tangaza bajeti ;wananchi mnasemaje?Kimya au kelele zetu ndio utakuwa usalama wetu?Kama wanakoishi wao mafuta yamepanda kwa zaidi ya shilingi 2000 je?Kigoma na Nkasi itakuwa shilingi ngapi?Kimya au kelele zitatusaidia?
Mshahara umeshapanda kwa kiwango chema kabisa?!Kimya au kelele zetu zitatusaidia?
Walimu kama watumishi wengine wa sirikali watapandishwa madaraja ya kazi ambayo sina hakika kama yataendana na kupandishwa kwa viwango vyo vya mshahara au Kimya au kelele zao zitasaidia?

Kuna neno katiba na kanuni za jumba la Dodoma ambazo zina ruhusu kutotoka nje ya maneno yaliyoandikwa ndani ya kitabu chenyewe.
Ujue si haki na usawa kukosoa kila kitu hasa wanapoangea Watanzania au wananchi wa nje yetu tanzia?

Tuesday, July 03, 2007

Marehemu alikuwa.....!

Marehemu alikuwa ni.............Sijui mimi nikifa nitapewa sifa ngapi na zipi?Hata ambao wanaojitambulisha kwa watu kama rafiki zangu kwa sasa niko hai waniambii mimi ni nani hasa?Kwa kuwa watu tumejaa na unafiki!... hata mimi mwenyewe nashindwa kujisemea; mimi hasa ni nani na nina sifa gani? katika jamii yangu....kama ni kibaka,mwongo,mla rushwa(UONEVU;WIZI;UUAJI),MVIVU(Sifundishi kama ni mwalimu na baka wanafunzi wangu,Daktari nabaka wagonjwa wangu,padri/sheikh nafanya uzinzi,ulawiti an uehserati na waumini wangu?) ;nashindwa kusema

Nahitaji fedha kwa sasa lakini hakuna hata mmoja kati yenu anayeniuliza mimi... unahitaji mkopo au fedha ili ......Hakuna!Hata mimi nashindwa kusema nahitaji fedha ili nifanye .........UNAFIKI.

Napenda kutembelea sehemu ambazo ni rahisiwatu kunitambua na kunipa sifa ...jana nilikuwa na fulani;nitembee sehemu zenye matatizo au kwa masikini ili aniombe fedha zangu kidogo nilizonazo....?hata wenye nchi hawawezi fika uko??nani?nani amefika TITYE tangia achaguliwe na fedha zake...?ndio fedha zake...na alipeleke gari lake....ambako barabara mbovu....wewe....

Najitahidi kumkumbusha kila siku Mola wangu ninachohitaji aniwezeshe niwe nacho.....Pia napenda kumwomba hata kifo changu kiwe cha kawaida ili watu wengine wasije pata kasheshe kwamba wao ndio chanzo cha kifo changu.

nakimbiza shilingi kwa umakini wa ajabu ili pia watu hasa rafiki zangu wasije sema jamaa alikuwa ki.....we acha! sisi ndio rafiki zake tulikuwa tunamjua jamaa.Njili alikuwa halali usiku.....wakati wao wako macho?
marehemu alikuwa ........

Amina kifo chako kingeweza kuepukika?AMINI.

Saturday, June 30, 2007

Kasulu

jana sio juzi!Ninge....Kamwe hakui kabisa.Maisha yako ukiyafananisha na ya fulani ;basi wewe sio wewe ila ni yeye.Hivyo basi hufai kuishi.Hapana Fulani mwenyewe hasiwe Yule ambaye jamii haimuhitaji kuwa naye!ISIWE FULANI KUWA WEWE!

Wednesday, December 20, 2006

MWISHO WA RELI-PICHANI

KIGOMA

NI SEHEMU TU YA KIGOMA PICHANI

Ni mwisho wa reli.Ni msemo ambao niliusikia takribani miaka zaidi ya Ishirini(20) na ushee tangia niishi hapa Tanzania;ndio hapa Tanzania?! na sio Tanganyika iliyotimizi miaka 45 ya Uhuru wake toka chini ya makucha?Tunamiriki maliasili zote sisi wewe?
Kuanzia Mara mpaka Mtwara ukipitia njia zote za lami majira yote ya mwaka.

Ndio Tanzania Bara?Watoto wake wanajua Uvinza kuna chumvi,Mikumi,Serengerti na Bonde la Moyowosi kuna wanyama pori na Gombe kuna Sokwe mtu.......Lakini atafikaje? kwani kutoka Tanzania mpaka Kigoma ni siku si chini ya tatu?

Mazingira yake yanachomwa sana kwa moto na acha hukataji wa mti.Niko huku sasa ni mwaka wa tatu nimeshaambiwa si na mtu mmoja ...........una ona ule mlima pale.....ule kule kuliko na msitu na wanyama pori kibao(wengi sana).

Wakimbizi walipoingia..............mafuta ya taa yaliporipuka bei...na sio kupanda;kwani zaidi ya asilimia 97 ya wenyeji wanatumia kuni?